Hotuba mbalimbali zilitolewa zikibainisha nafasi ya Imam Reza (a.s) katika kudumisha elimu na uongozi wa kiroho katika Uislamu.

25 Agosti 2025 - 09:26

Majlisi ya Kumbukizi ya Kifo cha Imam Reza (a.s) Yafanyika Kariakoo, Jijini Dar-es-Salaam +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar-es-Salaam - Tanzania - Majlisi maalumu ya kumbukizi ya kifo cha Imam Ali bin Musa ar-Ridha (a.s) imefanyika katika mitaa ya Kariakoo, jijini Dar-es-Salaam, ambapo waumini wengi walikusanyika kwa mapenzi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake watoharifu (a.s).

Mahudhurio

Hafla hii ya maombolezo imehudhuriwa na:

  • Waumini kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar-es-Salaam.
  • Wapenzi na wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s).
  • Wanafunzi wa Chuo cha Kisayansi cha Jamiat Al-Mustafa (s), kilichopo Mbezi Beach – Dar-es-Salaam.

Majlisi ya Kumbukizi ya Kifo cha Imam Reza (a.s) Yafanyika Kariakoo, Jijini Dar-es-Salaam +Picha

Shughuli zilizofanyika

Katika Majlisi hiyo kulisomwa:

  • Aya za Qur’an Tukufu.
  • Nauha na Marsia za maombolezo,
  • Hotuba zilizobainisha nafasi ya Imam Reza (a.s) katika kudumisha elimu na uongozi wa kiroho katika Uislamu.

Majlisi ya Kumbukizi ya Kifo cha Imam Reza (a.s) Yafanyika Kariakoo, Jijini Dar-es-Salaam +Picha

Umuhimu

Majlisi kama hizi zinaendelea kudumisha:

  • Mapenzi ya Waislamu kwa Ahlul-Bayt (a.s),
  • Kuimarisha mshikamano wa kijamii na kiroho,
  • Kuelimisha vizazi vipya kuhusu historia ya Maimamu watoharifu (a.s).

    Majlisi ya Kumbukizi ya Kifo cha Imam Reza (a.s) Yafanyika Kariakoo, Jijini Dar-es-Salaam +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha